JINSI ya Kutuma Maombi JWTZ 2025 NA MFANO WA BARUA YA MAOMBI



JINSI ya Kutuma Maombi JWTZ 2025, Jinsi ha Kutuma Maombi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

 April 30, 2025 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ limetangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa kitanzania wenye Elimu ya kidato cha nne hadi Elimu ya Juu.

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI KWA MAKUNDI YOTE MAWILI 2025
Maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 hadi tarahe 14 Mei, 2025 yakiwa na viambatisho vifuatavyo:-

  • Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au nambari ya NIDA.
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya Shule na Chuo.
  • Nakala ya cheti cha JKT kwa waombaji waliomaliza mkataba wa kujitolea.
  • Nambari ya simu ya mkononi ya mwombaji.

MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAYO
Mkuu wa Utumishi Jeshini,
Makao Makuu ya Jeshi,
Sanduku la Posta 194,
DODOMA, Tanzania

 MFANO WA BARUA YA MAOMBI YA JESHINI

EDY HASHIM SHABANI,
S L P 65,
CHALINZE PWANI .
O1/05/ 2025

MKUU WA UTUMISHI
MAKAO MAKUU YA JESHI
S L P 194
DODOMA TANZANIA

NDUGU , MUHESHIMIWA

YAH:MAOMBI YA KUJIUNGA NA JESHI.

      Husika na kichwa cha habari hapojuu mimi ni Edy Hashim shabani mwenye umri wa miaka 19 nimemaliza elimu ya sekondari mwaka 2024 katika shule ya sekondari Dunda center.
Naomba kijiunga na jeshi la JWTZ pia nakuahidi kifanikiwa kuipata nafasi yakuwa mtumishi wa jeshi nitafanya kazi ya jeshi kwa umakini na ueledi wa haliyajuu zaidi.
Nitashukuru sana iwapo ombilangu litakubaliwa

E.H.Shabani


EDY HASHIM SHABANI


Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form